May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Uturuki aipongeza STAMICO katika ubunifu

Na David John,TimesMajira Online, Dar

BALOZI wa Uturuki nchini Tanzania Dkt.Mehment Guluioliu amelipongeza Shirikal la Taifa la Madini STAMICO kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye sekta ya madini na kwani kuna juhudi kubwa zimefanyika kwa kuwa wabunifu katika kuhakikisha wananchi wanafaidika la rasilimali hiyo.

Balozi Mehment ambaye leo amekuwa sehemu ya wageni ambao wametembelea Maonyesho ya Kimataifa 45 ya Sabasaba ambayo yanafanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa wilayani Temeke.

Amesema kuwa shirika la madini STAMICO wanafanya kazi nzuri sana huku akivutiwa na Mradi wa Nishati ya Makaa wa mawe ambao wameaza kutekeleza nakwamba mradi huo utaondoa uharibu wa mazingira.

“Mrari wa makaa ya mawe ni mradi mzuri na ni sahihi kwani pamoja na kuwa utafaa kwa matumizi ya majumbani lakini pia utaondo uhalibifu wa ukataji miti hivyo na badala yake watu watatumia nishati ya makaa ya mawe,” amesema

Balozii wa Uturuki nchini akisaini kitabu cha wageni kwenye Banda la Wizara ya Madini mara baada ya kutembelea Shirika la Taifa la Madini Stamico

Nakuongeza kuwa “Amefika kwenye Banda la STAMICO na kupongeza namna hata banda lao linavyovutia na kwamba hata katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu ambacho kimejengwa mkoani mwanza ni kazi nzuri sana ya shirika hili “amesema Balozi Mehment .

Amesema kuwa wao kama Uturuki wanaunga mkono juhudi kubwa ambazo zinaendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini Rais Samia Hassan Suluhu Kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania kwa ujumla.

Licha ya Balozi huyo wa Uturuki lakini pia viongozi mbalimbali na Balozi wanaowakilishi nchi zao hapa nchini walipata fursa ya kutembelea maonyesho haya ya Sabasaba na kujionea namna wajasiliamali na wafanyabiashara waliojitokeza.