Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, DSM
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Kattanga amekutana na ugeni huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sulluhu Hassan. Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) katika nyanja za biashara na uwekezaji pamoja na Ulinzi na Usalama.
Balozi Kattanga amemhakikishia Waziri huyo kuwa Tanzania inayo mazingira mazuri ya biashara na salama kuwekeza.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoka kwa Umoja huo wakati wote.
Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan amewasili nchini leo kuja kushiriki Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru