Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma
KAIMU Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) nchini, Deodatus Balile amewataka wahariri na waandishi wa habari kwa ujumla kusimamia maadili na taaluma yao badala ya kuingia kwenye mitego ya kutaka vyama vya siasa kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akizungumza Jijini Dodoma leo na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TEF utakaofanyika kwa siku mbili ambapo pia utafanya mapitio ya utendaji wa vyombo vya habari mwaka uliopita na kuweka mipango ya mwaka huu Balile amesema,jukumu la mwandishi wa habari kulinda na kufuata misingi ya taaluma yake na siyo vinginevyo.
Amesema kipindi hiki cha uchaguzi ndio wakati ambao waandishi wa habari wanapaswa kufanya kazi kwa ufanisi huku wakitambua zipo sheria zinazowaongoza na zinafanya kazi.
“Kipindi hiki cha uchaguzi malalamiko ni mengi ,tusiyapuuze bali tuangalie namna ya kuyashughulikia ,lakini vyombo vya habari havipaswi kutumika kutukana wengine au kwa uchochezi,’ amesema Balile
More Stories
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi