Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
KATIKA kuhakikisha wapenzi wa Filamu wanaelimika na kuburdika chaneli ya Sinema zetu kupitia kisimbuzi cha Azam Tv imezindua tamthilia mpya inayoitwa Siri .
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Sinema Zetu, Sophia Mgaza amesema tamthilia ya siri inausisha visa na mikasa wanavyovipitia madereva teksi kwa kutumia programu tumishi ili kupata wateja .
Sophia amesema tamthilia hiyo inatarajiwa kuoneshwa Disemba Mosi mwaka huu katika chaneli ya Sinema zetu katika kisimbuzi cha Azam Tv kuanzia ijumaa mpaka jumapili saa moja usiku.
“Tamthilia hii inamlenga msichana mmoja aitwaye Sophia anajikuta katika matatizo makubwa baada ya mteja asiyejulikana kutelekeza maiti katika gari lake pasipo yeye kifahamu”amesema Sophia
Aidha Sophia amesema kitendo cha dereva huyo kususiwa maiti katika gari lake pasipo yeye kufahamu kinasababisha mikasa na kadhia inayosimuliwa Kwa namna ya kuvutia huku picha zake za mnato zikinaswa na kamera na vinasa saut vya kileo .
Naye Muandaaji wa tamthilia hiyo kutoka Irene Paul amesema tamthilia hiyo imebeba visa na mikasa vinavyoendana na maisha ya halisi ikiwa na lengo la kuelimisha na kuburudisha.
Alisema katika tamthilia waigizaji waliohusika ni pamoja na yeye mwenyewe Irene Paul, Neema walele, Habibu Mtambo, Prince Jimmy, Salha Abdallah, Salim Yakuti, Mayasa Mrisho, Zainab Ally, Shafii Bashiri, Christina Rogat pamoja na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Tanzania.
Tamthilia ya Siri inachukua nafasi ya tamthilia ya mchogo itakayofikia tamati Novemba 25 .
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu