January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Auawa na kundi la tembo katika mapambano

Na Steven Augustino, Tunduru

MKAZI wa Kijiji cha Angalia wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, Rajab Aweje Kapilipili (43) amefariki dunia baada ya kushambuliwa na kundi la tembo.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa, marehemu Kapilipili alikubwa na mkasa huo wakati akijaribu kuwafukuza tembo hao ambao walivamia shamba lake.

Walisema, katika tukio hilo marehemu alikanyagwa kanyangwa na kupasuka pamoja na kuvunjika viungo vya sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa, tukio hilo lilitokea April 27, mwaka huu majira ya kati ya saa 2.30 usiku katika Kijiji cha Chikunja eneo la Mto Mwambesi.