May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Atletico Madrid, Inter Milan zajiondoa Ligi Kuu Ulaya

MADRID, Uhispania

KLABU ya Atletico Madrid inayoshiriki Ligi Kuu Uhispania (La Liga) na Inter Milan ya Italia wamezifuata Manchester City, Chelsea, Liverpool, Arsenal, Tottenham Hotspur na Manchester United kujiondoa kwenye Ligi Kuu ya Ulaya (ESL ) iliyopendekezwa kufanyika hivi karibbuni.

Manchester United, Liverpool, Arsenal na Tottenhamm jana nao walitanga kujiondoa kwa kuungana na Chelsea pamoja na Manchester City ambao wote wanashiriki Ligi Kuu England kujiondoa kwenye Mpango wa European Super League.

Man City, ndio walikuwa wa kwanza kuthibitisha hadharani kwamba walikuwa wamejiondoa kwenye mashindano hayo juzi jioni, licha ya habari hapo awali kuripoti Chelsea mapema siku hiyo walikuwa wamepanga kujitoa.

Kwa mujibu wa waandaaji wa Supa Ligi, jana imesema watafikilia hatua zinazofaa zaidi kurekebisha Mpango wao. Huku ikitajwa kuwa wanataka kuachana na klabu hizo amabozo zimeamu kujitoa.

Hata hivyo, Ligi Kuu Ulaya (ESL), imekosolewa tangu kutangazwa mwishoni mwa wiki, ambapo takribani mashabiki 1,000 walikusanyika nje ya uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge kabla ya mchezo wao dhidi ya Brighton kupinga kuhusika kwao Kwenye Mashindano hayo.

Chelsea na Man City walikuwa sehemu ya vilabu “vikubwa sita” vya mpira wa miguu huko Uingereza pamoja na Arsenal, Liverpool, Manchester United na Tottenham ambao wote walikubali kujiunga na ligi hiyo mpya.

Jumla, vilabu 12 vya Ulaya vilitangaza nia yao ya kuunda ligi ambayo inaelekea kuvunjwa, ambayo walitarajia kuanzisha kama mashindano mapya katikati ya wiki. Mashindano yamepingwa na mamlaka za mpira wa miguu na mawaziri wa serikali nchini Uingereza na kote Ulaya na UEFA na vyama vya Soka mbalimbali, Timu na wadau wa Soka.