December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ATCL yarejesha safari za Dar es Salaam, Guangzhou

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) Leo imesheherekea urejeshwaji wa safari zake za Dar es Salaam kwenda Guangzhou kwa kusafirisha ujumbe wa makampuni 25 yanayoongoza kwa watalii nchini China.

Ujumbe huo umeambatana na vyombo 6 vya habari mashuhuri kutoka nchini humo na umewasili na Air Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume, Zanzibar ukitokea Guangzhou, China.