Na David John, TimesMajira Online
ASKOFU wa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Jackson Sosthenes amewataka vijana wote nchini hasa wa kanisa hilo kujiandaa kikamilifu kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika Agosti mwaka huu.
Akizungumza wakati akifungua semina Maalum ya vijana wa kanisha hilo Dayosisi ya Dar es Salaam ( TAYO) iliyofanyika Kanisa la St.Andrew Magomeni,Askafu Jackson amesema pamoja na mambo mengine huu ni mwaka wa sensa Kitaifa,hivyo ni vema tuhamasishana na kisha kushiriki katika sensa hiyo kwani ni Jambo muhimu sana katika Taifa ambalo linafanya watawala kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo .
Amesema uwepo wa sensa unafanya Serikali kujua idadi ya watu wake na vitu mbalimbali vilivyopo ambavyo vinauzunguka jamii husika na kwamba Taifa lolote duniani linahitaji kujua idadi ya watu wake ili kupanga mipango yake ya kimaendeleo na ili kufanikisha hilo kunahitajika uzalendo watu katika kujjitokeza na kushiriki katika matukio muhimu katika nchi Kama sensa.
“Tnafahamu Agosti mwaka huu nchi yetu inaingia kwenye jambo kubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili,tutakuwa na sensa ya watu na Makazi,niwaombe vijana wote nchini mkiwemo wa Kanisa la Anglikana kuhakikisha mnashiriki kwa vitendo, Serikali ikiwa na takwimu kamili ya watu wake pamoja na vitu vilivyopo ni rahisi kuweka mipango ya maendeleo,”amesema Askofu Jackson.
Ameongeza kwamba ipo changamoto ya baadhi ya vijana wa Kanisa kutokuwa wazalendo hata ndani ya Kanisa kwa kutosimamia vema kazi mbalimbali ya Kanisa hilo wanazopatiwa,hivyo katika hili la sensa wote tukaweka uzalendo mbele kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
Kuhusu semina Askofu Jacskon amewakimbusha vijana wa Kanisa hilo kuendelea kuwa waadilifu na wenye kujenga umoja,upendo na mshikamano katika inayowazunguka na Kanisa kwa ujumla huku akiwapongeza vijana hao wa kuandaa semina hiyo iliyoambatana na matukio mbalimbali likiwemo la kuliombea Taifa na viongozi wake.
Aidha semina hiyo imejenga msingi wa kuendelea kuwaleta pamoja vijana wote kwa ajili ya kufungua mwaka mpya wa 2022 lakini pia kufanyika kwa Maombi ya pamoja kwa ajili ya Kanisa na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu wa Umoja wa Vijana wa Kanisa hilo Padre John Upio amewakumbusha vijana hao umuhimu wa kushiriki semina na makongamano yanayoandaliwa na Kanisa yenye lengo la kutambuana na kuwakumbusha majukumu yao katika Kanisa.
Pia amepata nafasi ya kuelezea kalenda ya Kanisa ya mwaka huu yenye matukio mbambali ya vijana ,hivyo ushiriki wao kwenye matukio hayo kadri yatakavyokuwa yanajitokeza ni muhimu wakawepo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best