January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim Pentekoste Peter Konki

Askofu awataka waumini kuombea Uchaguzi Mkuu

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Elim Pentekoste Peter Konki amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuombea Uchaguzi Mkuu na wagombea wote hususa Rais John Magufuli kwani ndiye Rais aliyepo madarakani kwa sasa.

Akizungumza katika ufunguzi wa Makao makuu ya ofisi ya Kanisa hilo yaliyopo Ihumwa jijini Dodoma Askofu Konki amesema ,wagombea wote kuanzia ngazi ya kata mpaka urais wanahitaji maombi lakini Dkt.Magufuli anahitaji zaidi ili Mungu amlinde na kumtumza kwani mbali na kuomba kura bado ana majukumu ya urais anayoyatekeleza.

“Tunahitahi sana kumwombea Rais ,pamoja na kwamba na yeye ni mgombea ,kama utamlinganisha a wagombea wengine utakuwa umefikiri tofauti,yeye ni taa ya Tanzania na ngao yetu.”

Amesema Askofu Konki na kuongeza “Tusielewane vibaya ,hakuna chama ninachokitetea bali nasimama katikati.”

Amesema wakati huu wa uchaguzi ni muhimu sana waumini kuombea wagbea na nchi kwa ujumla ili mchakato huu uishe salama na kuiacha nchi katika hali ya utulivu na amani .

Kanisa la Elim Pentekoste lilikuwa na makao makuu yake mkoani Tanga lakini kutokana na ujio wa Makao Makuu mkoani Dodoma ,kanisa hilo lilifikia uamuzi wa kuhamishia makao makuu ya Kanisa jijini Dodoma kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kuhamishia makao makuu mkoani Dodoma.