November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Pamoja ya Maaskofu na Mashekh ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini zote nchini, Askofu William Mwamalanga,

Askofu awachongea kwa Rais Samia watetezi tozo mpya miamala ya simu

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online,Dar

ASKOFU William Mwamalanga amempongeza Rais Samia kwa kusikilikiza vilio vya wananchi kutokana gharama kubwa za miamala ya simu, huku akishauri wachukuliwe hatua waliokuwa wakishangilia tozo hizo.

Taarifa ya Askofu Mwamalanga kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo imeeleza kuwa tozo kubwa kwenye miamala ya simu zimechafua taswira ya ustawi wa nchi yetu, kwani zimesababisha vilio nchi nzima, huku dunia nzima ikielekeza macho yake kwa Tanzania.

Amesema ni vema akatumia macho mapana kuliangalia jambo hili, kwani lingeweza na kutengeneza chuki na wananchi.

MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Pamoja ya Maaskofu na Mashekh ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini zote nchini, Askofu William Mwamalanga,

“Ni busara kuwaondoa kwenye nyadhifa zao wale mawaziri ambao walikuwa wakishangalia na kuita tozo hizo zinakwenda kutengeneza barabara, madarasa na vituo vya afya, jambo lilichukiza sana wananchi,”amesema.

Aidha, Askofu Mwamalanga amemshauri Rais Samia asiishie kurekibisha tozo kwenye miamala ya simu pekee yake, badala yake aende mbele zaidi kwa kupunguza bei za mafuta ya petrol na diseli, kwani zikiachwa kama zilivyo kwa sasa zitasababisha kuyumba kwa kilimo na kusababisha mfumuko mkubwa bei.

Amesema hatua hiyo inaweza kutengeneza umasikini na kuimarisha matabaka ya wenye nacho na wasiyo kuwa nacho.

Hata hivyo Askofu Mwamalanga ameshauri Serikali kuajiri wabobezi wa kiuchumi wasiotokana na vyama vya siasa ili kuendana na uchumi chanya kwenye madini, kilimo na utali maeneo ambayo yanatosha kuinua maendeleo na uchumi wa taifa.

“Hivyo napendekeza kufuta tozo zote kwenye simu na badala yake kodi hizo wakatwe wabunge na mawaziri,”alisema.