December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya biashara ya danguro

Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza

Mfanyabishara James Chacha(58), Mkazi wa Iloganzara wilayani Ilemela mkoani Mwanza amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya biashara ya danguro kwenye nyumba yake.

Akizungumza jijini Mwanza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, ameeleza kuwa Juni 2,2923 majira ya saa 3 na dakika 40 usiku huko maeneo ya Sabasaba Kata na Wilaya ya Ilemela walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anafanya biashara ya danguro kwenye nyumba yake.

Pia katika nyumba hiyo walikamatwa watuhumiwa 53 kati yao wanawake 23 na wanaume 30 wakifanya vitendo vya ngono kinyume na maadili.

Mutafungwa ameeleza kuwa mnamo Juni 2,2023 majira ya saa 2 na dakika 30 asubuhi Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa eneo la Iloganzara karibu na shule ya msingi Tulele @ kwa Chacha kuna biashara ya danguro.

Baada ya taarifa hizo kuripotiwa askari walifanya ufuatiliaji ambapo walifika eneo hilo nakufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi ukikamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.