January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Anjella: Wasanii tupambane

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

CHIPUKIZI wa muziki wa Bongo fleva kutoka Kondegangs, Anjella amesema wasanii wanatakiwa kupambana katika muziki iii waweze kufika pale wanapotaka.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Anjella amesema,kila kitu kinapangwa na Mungu hata kama kina changamoto cha msingi kutokana tamaa.

“Kila kitu kinachotokea ujue Mungu amekiruhusu hata kama kiwe na changamoto kiasi gani, tunachotakiwa ni kupambana hadi tufike tunapotakiwa kufika, hakuna kukata tamaa,” amesema Anjella.