January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Angola yaendeleza ubabe kwa Zanzibar, CANAF 2021

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Angola, Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Afrika kwa mchezo wa soka kwa wenye Ulemavu CANAF 2021
wameonyesha kwamba wao ni mabingwa baada ya kuichabanga Zanzibar 12-0 Uwanja wa Uhuru leo, Novemba 28, 2021.

Katika kipindi chote Angola waliutawala mchezo huo kutokana na uzoefu mkubwa wa wachezaji wao wanaocheza katika mashindano ya kimataifa.

Kipindi cha kwanza tayali Angola ilikuwa inaongoza kwa magoli sita kwa nunge na katika kipindi cha pili wakaongeza magoli mengine sita na kufanikiwa kupata ushindi wa dazani moja dhidi ya Zanzibar.

Magoli ya Angola yamefungwa na Kufula Hilario, Aharo Francisco, Joachim Sabino, Chiarere Jord na Pacincia Fblio.

Mashindano haya yamezinduliwa rasmi jana Novemba 27 na yatakamilika Disemba 4, 2021.