Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa msimu mpya wa michuano ya kabumbu ulimwenguni kote, Kampuni ya michezo ya kubashiri Parimatch Tanzania imekuja na kampeni yao ya Amsha Mzuka yenye lengo/dhumuni la kuwawezesha wateja wake na wadau wote wa kubeti kufurahia msimu huu wa soka kwa kujipatia zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja ‘Smartphone’ pamoja na fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni moja kila siku.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Masoko wa Parimatch Tanzania, Levis Paul wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo na kusema kuwa Promosheni hiyo ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hichi cha Ligi zinaporudi.
Aidha, Levis amesema kuwa lengo kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe kutoka kwako katika kipindi hichi ambacho soka linarejea viwanjani ulimwenguni kote.
“Katika kipindi cha kuanzia 09.08.2023 hadi 08.09.2023, mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wowote kupitia tovuti yetu www.parimatch.co.tz au app zetu basi ataingia moja kwa moja katika droo wa kuwania pesa taslimu kiasi cha Milioni Moja za Kitanzania pamoja na smartphone aina ya Samsung mpya (Simu janja)”, alisema Levis.
Aidha Levis aliendelea kwa kusema kuwa “Kila siku tutakuwa tunatoa zawadi ya simu kwa washindi husika na Zawadi ya pesa itatolewa kila baada ya siku ya moja kupita. Washindi wote wanatangazwa kupitia Clouds fm katika kipindi cha michezo pamoja na kurasa zetu za kijamii kwa siku husika”.
Pamoja na hayo, Levis amefafanua kuwa ili uweze kukidhi vigezo vya kushiriki kampeni hiyo mshiriki anapaswa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na kuendeleeaKampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao! Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual.
Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM