April 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Aliyeibuka ghafla kumpelekea bahasha Rais ahojiwa na polisi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la polisi mkoani Dodoma limemuhoji mwananmke mmoja aliyetambulika kwa jina la Veronica Raphael (41) mkazi wa Dodoma mjini ambaye siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ,aliibuka ghafla akiwa amebeba bahasha na kutaka kuipeleka moja kwa moja kwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa akihutubia wananchi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani humo Februari 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amesema utaratibu huo ni kinyume na taratibu kwani Rais anao wasaidizi wake waliopaswa kupewa ujumbe ule na wao ndio waufikishe kwa Rais.

Hata hivyo kabla mwanake huyo kabla hamfikia ,Rais alielekeza bahasha ile wapewe wasaidizi wake.

Kamanda Lyanga amesema hatua ya mwanamke hiyo ilizua taharuki katika itifaki za kiusalama na hivyo jeshi la polisi likafanya kazi ya kumhoji ili kujua yeye ni nani na baada ya kuangalia nyaraka zake,walienda hadi mahakamani kupata taarifa kuhusu ukweli wa malalamiko yake ambapo alidai kuwa mahakama imemtapeli  gari lake.

Hata hivyo taarifa kutoka mahakamani ilieleza kuwa ni kweli Veronica alikuwa na kesi mahakamani ambayo tayari ilishafanyiwa maamuzi na alishakata rufaa lakini bado alishindwa katika kesi hiyo .

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya mahakama bado Veronica anayo nafasi ya kukata rufaa ngazi za juu zaidi kama anaona bado hajaridhika badala ya kukimbilia kwa Rais moja kwa moja.

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuacha kukimbilia kwa viongozi wa juu wakati wanao uhuru wa kukata rufaa kwenye vyombo vinavyohusika na changamoto zao kupatiwa ufumbuzi.

“Nawaomba wananchi msipende kukimbilia juu suala liko wazi Mahakama.zipo na Jeshi lipo msipende kuwadanganya viongozi,”alisema Kamanda Lyanga na kuongeza kuwa

“Kwa mfano kabla ya kilele cha maadhimisho haya kulikuwa na wiki ya sheria ambayo iliandaliwa na mahakama na kulikuwa na mabanda mbalimbali yakiwemo ya msaada wa kisheria katika viwanja vya Nyerere,lakini taarifa zinaonyesha huyu Veronica hakuwahi kufika pale kupata msaada wa kisheria na badala yake akasubiri kukimbilia kwa Rais.”