January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Alhaj Othman,ashiriki maziko ya mama wa Waziri wa fedha na mipango Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman,Agosti 27, 2024 amejumuika pamoja na Viongozi Wakuu, Masheikh, na Waumini mbalimbali wa Kiislamu, katika Maziko ya Marehemu Mvita Mussa Kibendera.

Marehemu Mvita,alifariki Dunia usiku wa kuamkia Agosti 27,2024,ambaye ni Mama wa Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dokta Saada Mkuya Salum,amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Sala imeongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, Msikiti wa Ijumaa Mwembeshauri,na amezikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa na jamii, wamehudhuria maziko hayo wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dokta Hussein Ali Mwinyi