Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka jamii kuhakikisha inaweka mipango madhubuti itakayowafanya vijana balehe wa kike kutojiingiza katika ngono ili kuzuia mimba katika umri mdogo lakini pia wafikie nalengo yao hasa kuhitimu masomo yao.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo leo katika hafla ya kuzindua Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo kwa vijana balehe huku akisema, kama vijana hao wa kike wataendelea kujihusisha katika ngono ambayo huathiri masomo yao kwa kupata mimba, hata elimu bila malipo inayotolewa na Serikali haitakuwa na maana.
“Vijana wamepata fursa ya kupata fursa ya kupata elimu bila kikwazo, lakini jitihada hizo hazitakuwa na tija kama walengwa hawatahitimu masomo, matarajio ya Serikali ni kuona idadi ya watoto ya kuingia shule na kutoka inakuwa sawa.”alisema na kuongeza kuwa
“Kwa mujibu wa sense ya Watu na Makazi nchini yam waka 2012 pamoja na makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2020 lakini pia idadi ya vijana balehe wenye umri kati ya 10-19 iliyofikia milioni 13.206 sawa na asilimia 22.9 ya watu wote nchini wanaingia kwenye mpango huu” Waziri Mkuu
Aidha amesema kati ya vijana wa kiume milioni 6.597 sawa na asilimia 49.94 na vijana wa kike milioni 6.609 sawa na asilimia 90.05 na kwamba takwimu hizo zinaonyesha kwamba vijana ni kundi kubwa linahitaji kuwekezwa katika kuhudumiwa.
Amewataka wadau wote zikiwemo wizara za kisekta kuwajibika katika kulitunza na kuliangalia kwa karibu kundi hili la vijana balehe huku akisema kwa upande wan Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba changamoto zinazolikabili kundi hilo zikiwemo kuambukizwa magonjwa, upungufu wa taaluma na kujiajiri ,matumizi ya dawa za kulevya, ukatili wa kijinsia ndoa na mimba za utotoni vinapatiwa ufumbuzi.
Akizungumza kwa niaba ya kundi la vijana balehe Nzengo Nsumi (15) mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka wilaya ya Ikungi mkoani Singida amesema, ajenda hiyo inabebwa na nguzo kuu sita huku akifafanua nguzo ya kwanza ya kuzuia maambukizi ya ukimwi kwa kundi la vijana balehe.
Amesema, takwimu kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti maambukizi ya Ukimwi (TACAIDS) ya mwaka 2019 inaonyesha kuwa maambukizi mapya ni milioni 3.058 na kati ya hao asilimia 50 ni vijana balehe ,na kwamba katika hiyo asilimia 50 ya vijana balehe asilimia 80 ni vijana balehe wa kike na asilimia 20 ni vijana balehe wa kiume .
“Hii inaonyesha kuwa vijana balehe wa kike wanaambukizwa zaidi kuliko vijana wa kiume “alisema Nsomi na kuongeza kuwa
“Katika nguzo hiyo kuna afua za kipaumbele tatu ambazo zimelenga kuziuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana hao ambapo afua ya kwanza ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa wigo wa upimaji virus vya ukimwi kwa vijana balehe,
“Afua ya pili ni kuwawezesha vijana wa kike na wa kiume kutumia mbinu sahihi zitakazowasaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi ambapo mbinu hizo zinatakiwa ziambatane na mafunzo mbalimbali yatakayowasiaidia vijana hao kujikinga na maambukizi ya virus hivyo.
“Na Afua ya tatu ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya tohara kwa vijana wa kiume ambapo takwimu mbalimbali zinaonyesha vijana wakipata huduma hii ya tohara inawasiadia kujikinga dhidi ya maambukizi ya virus vya ukimwi kwa asilimia 60.
Kwa upande wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema lazima Serikali iwekeze nguvu nyingi hasa kwa vijana balehe hasa wa kike ili kuwa na wamama wajao wenye afya njema.
Aidha alisema Chimbuko la ajenda hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya Virus vya Ukimwi na mimba za utotoni kwa vijana balehe .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa