December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ahukumiwa kifo kwa kubaka wajukuu

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Sumbawanga

MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imemuhukumu kifungo cha Maisha jela, Joseph Nyansio (40) mkazi wa Kijiji cha Kasekela wilayani Sumbawanga baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuwabaka wajukuu wake wawili.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Shadrack Masija ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Jana na kusema kuwa watoto hao (majina yamehifadhiwa) walikua na umri wa miaka 7 na mwingine miaka 8.

Amesema kuwa siku ya June 29 mwaka huu majira ya mchana, mtuhumiwa huyo aliwalaghai watoto hao kuwa anawapeleka shambani ili akawachumie matunda ndipo alipo wafanyia kitendo hicho.

Kamanda huyo amesema kuwa baada ya mtuhumiwa kukamatwa na upelelezi kufanyika ndipo alipofikishwa mahakamani mbele ya hakimu Thomas Bigambo na baada ya ushahidi kukamilika, siku ya Octoba 30 alihukumiwa kifungo cha Maisha jela.
No
Aidha Kamanda Masija akitoa wito kwa wanaume mkoani humo kuacha kuendekeza tamaa za kimwili ndiyo imekua sababu ya kuwafanyia matukio ya kikatiri watoto pamoja na ndugu zao na kuishia kupata adhabu Kari.

Pia amewataka wananchi kuacha Imani potofu za kishirikina kwani zimekua chanzo kikubwa cha maovu mkoani humo badala yake wajitume kufanya kazi ili wapate mafanikio halali katika Maisha yao.