Na Mwandishi wetu,timesmajira ,Online
WANANCHI wa Mkoa wa Pwani wanatarajia kuanza kupata matibabu katika kituo kipya cha Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan Tanzania.
Taasisi hiyo imefungua kiliniki ya kwanza ya kisasa inayotoa huduma za awali za kitabibu na afya katika mkoa huo.
Mkurugenzi wa Vituo vya Aga Khan Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Mashariki ya Kati, Shakir Bandali amesema ufunguzi kituo hicho ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza miaka 91 toka kuanzishwa kwa taasisi hiyo kupitia muongozo wa mtandao wa maendeleo wa Aga Khan (AKDN).
Amesema miongoni mwa huduma zitakazo tolewa ni pamoja Digital X-Ray, Ultrasound, maabara, kifamasia, kliniki za madaktari bingwa wa watoto, upasuajina kinamama pamoja na kliniki ya afya ya mama na mtoto zitakazo tolewa na kituo hiki.
“Dhamira ya taasisi yetu ni kutoa ni kufikisha na kusogeza huduma bora, angalizi, nafuu, na za uhakika kwa Watanzania wote pasipo kujali rangi, dini, kabila wala tabaka kwa kujenga vituo vilivyofika ngazi ya wilaya na kuwezesha huduma za matibabu kwa wenye mahitaji kupitia bima ya afya ya taifa (NHIF) na bima zinginezo”Amesema
Aidha amesema kituo hicho cha kwanza cha Afya Aga Khan Polyclinic katika Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani,kinakuwa cha 23 kufunguliwa ndani ya tika kip miaka sita na kwa sasa katika mkoa waPwani Taasisi hiyo ina mpango wa kuongeza vituo kadhaa vidogo (Mini-clinic).
Amesema kufunguliwa kwa kituo hicho kinacho fanya kazi chini ya uangalizi wa hosipitali Taasisi hiyo ya rufaa itatoa huduma za awali za tiba kwa wakazi wa Kibaha na maeneo ya jirani na kuondoa changamoto za kufuata huduma hizi katika hospitali za kubwa za Mkoa
“Uwekezaji huo umegharimu dola za Marekani 150,000 sawa na Shilingi milioni 345 kwa kujenga mfumo wa kisasa wa kutoa huduma za radiologia (yaani PACS) na upatikanaji wa madaktari bingwa kwa njia ya electroniki/mtandao yaani teleconsultation,”amesema na kuongeza
“Uwekezaji huu ni mchango katika ukuaji wa uchumi na pia katika kufungua milango ya ajira kwa vijana wetu wa Kitanzania, kwa kuzingatia kwamba kituo kimoja cha afya kinatengeneza na kuibua fursa za kada mbali mbali wastani wa ajira 15 – 20 za moja kwa moja,”amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Aga Khan Tanzania, Sisawo Konteh amesema taasisi hiyo inaendelea kushirikiana na serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto katika kuatekeleza mradi mkubwa wa afya ya mama na mtoto uliosanifiwa kwa mwaka 2017-2021 ukigharimu shilingi bilioni 27 za Kitanzania ($12million) na kutekelezwa katika wilaya nane za mkoa wa Mwanza.
More Stories
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru
Msigwa aagiza ukamilishwaji wa haraka nyaraka muhimu za uanzishwaji wa bodi ya Ithibati ya waandishi wa habari
Mikopo ya ZEEA yaanza kutolewa kidijitali, maofisa washauriwa kuwa makini