May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

AfrONet wapongeza uteuzi wa Dk Mwatima

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MTANDAO wa Kilimo Hai Afrika (AfrONet), umempongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Dkt Mwatima Juma kwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Baraza la Kumshauri Rais kuhusu Utekelezaji wa Masuala ya Kilimo na Chakul.

Rais Samia ameunda baraza hilo Machi 14, 2023, ikiwa ni kutekeleza azimio la viongozi wa Afrika, kupitia Mkutano wa Utoshelevu na Ustahimilivu wa Chakula (Dakar 2 Summit on Feed Africa, Food Sovereignty and Resillience) uliofanyika Dakar Senegal kuanzia Januari 25 hadi 27, 2023 ambao ulihimiza kila nchi kuunda baraza la kusimamia utekelezaji mkakati wa kukuza kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula.

Pamoja na Dkt Mwatima wajumbe wengine Sekretarieti ni Katibu Mkuu mstaafu na Mwahadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dkt Florence Turuka na Mkurugenzi Mtendaji wa Mazao ya Mbogamboga Tanzania (TAHA) Dk Jacqueline Mkindi.

Kwa upande wa wajumbe wa Baraza hilo Rais Samia amemteua Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye ni Mwenyekiti, Mkurungenzi Mtendaji wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga na Katibu Mkuu mstaafu Andrew Massawe.

Akizungumzia uteuzi huo Rais wa AfrONet Josephine Atangana, alisema mtandao huo unampongeza Dk Mwatima kwa kuaminiwa na Rais na matumaini yao ni kuona uwakilishi sahihi kwenye sekta ya kilimo na chakula.
Atangana amesema AfrONet ina matumaini makubwa kwa Dk Mwatima na kuahidi kuwa watampa sapoti na ushirikiano wakati wowote katika majukumu mapya ambayo amepata.
“Uteuzi wako ni ushahidi tosha, kuhusu kazi zako kwenye mchango wako katika sekta ya kilimo hasa kilimo hai,” amesema,” Atangana.

Amesema Dk Mwatima, ambaye ni Mwenyekiti wa TOAM wanatarajia atakuwa na ushauri wenye mwelekeo chanya katika kufanikisha malengo ya Dakar 2.

“Uteuzi huu tunaouona kwa mtazamo changa katika kuendeleza kilimo hai Tanzania na Afrika.

Akiwa kiongozi wa TOAM, Dkt Mwatima ameonesha dhahiri kuwajibika na kuelekeza katika kuhamasisha kilimo hai Tanzania hali ambayo imeboreha maisha ya wakulima.

Rais huyo wa AfrONet amesema Dkt Mwatima ana nafasi kubwa ya kufikisha sauti na mahitaji ya wadau wa kilimo hai kwa kuzingatia maazimio ya Dakar 2