May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba

Adaiwa kumjeruhi mumewe kwa kisu

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MKAZI wa Uzogore Kata ya Ibadakuli, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amejeruhiwa kwa kukatwa na kisu sehemu za ubavuni kulia na mkewe baada ya kutokea ugomvi kati ya wanandoa hao.

Tukio hilo ni la pili kutokea mjini hapa ndani ya wiki moja la wanawake kuwajeruhi waume zao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amemtaja mwanaume aliyejeruhiwa kuwa ni Mpemba Gamba (48) na kwamba tukio hilo lilitokea saa sita usiku wa kuamkia jana baada ya kutokea ugomvi kati yake na mkewe aliyetajwa kwa jina la Suzana Richard mkazi wa Uzogore.

Amefafanua kuhusu tukio hilo, Kamanda Magiligimba alisema chanzo cha ugomvi kati ya wanandoa hao ni mwanamke kulazimisha kuendelea kuishi na mumewe baada ya kuwa amefukuzwa kwa kosa la kushindwa kumpikia mumewe.

Pata habari hii kwa kina kwenye Gazeti la Majira…