Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma
MAKAMU Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Zanzibar, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Othman Masoud Othman, leo Jumamosi Januari 13, 2024 amewaongoza Viongozi mbali mbali, katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, wa Chama chake, Mkoa wa kichama wa Kaskazini ‘A’ Unguja.
Hafla hiyo ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ni Mfululizo wa Mikutano anayoendelea kuiongoza Mheshimiwa Othman, ili kufanikisha Zoezi la Uchaguzi wa Ndani ya ACT-Wazalendo, Nchini kote.




Kwa upande wa Kaskazini Unguja, Mkutano huo wa Uchaguzi una dhamira ya kuwapata Viongozi Wapya watakaokitumikia Chama hicho kwa Kipindi cha Miaka Mitano (5) ijayo, katika Ngazi ya Mkoa.
Katika Mkutano huo wamehudhuria pia Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Ndugu Hassan Jani Masoud na Katibu wa Uchaguzi Ndugu Muhene Said Rashid.






More Stories
Upatikanaji wa maji Chunya wafikia asilimia 52
MiXX Yakabidhi Zawadi kwa Washindi wa Kampeni ya Kombe la Dunia
Mwenge wazindua jengo lenye thamani ya bil 3.4