May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

AATI yazindua ofisi ya mabadiliko ya kilimo Tanzania

Na Prona Mumwi,Dar es Salaam

WIZARA ya Kilimo kwa kushirikiana na Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo ( African Agricultural Transfomation Initiative- AATI) wazindua ofisi ya Mabadiliko ya kilimo Tanzania, Agricutural, Transfomatin Office (ATO)

Uzinduzi huo umefanyika Septemba 05, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa pembeni katika kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Septemba 05 hadi 08, 2023.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo, Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa ofisi ya ATO itasaidia mabadiliko ya kilimo cha Tanzania na kuwa na sekta jumuishi, endelevu, na inayoendeshwa na ujuzi inayostahimili tabianchi.

Ameema kuwa ATO itakuza mageuzi na ukuaji wa sekta ya kilimo nchini kupitia dira ya utekelezaji wa mikakati, kuongeza uwezo wa Serikali katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Mabadiliko ya Kilimo, na kusaidia utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Mabadiliko ya Kilimo kwa ufanisi na utekelezwaji wa kina.

Pia Waziri Bashe amesema Ofisi pia itasaidia katika kujenga uwezo (ikiwa ni pamoja na uwezo na zana za kidijitali) na kupeleka zana za ufuatiliaji na tathmini katika maeneo ya husika.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji, Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo Afrika (AATI), Safia Boly amesemaTukio la kando la litaangalia hali ya sekta ya kilimo na njia ambazo ofisi ya ATO iliyotengenezwa kuendeleza juhudi za Serikali.

Tukio la uzinduzi limetoa elimu kuhusu juhudi za Tanzania za kuharakisha mageuzi ya uchumi wake kupitia uimarishaji wa taasisi zake na ushirikiano na sekta binafsi, na kuboresha kubadilishana maarifa na kujifunza kuhusu changamoto, fursa na njia ya kusonga mbele kwenye mabadiliko ya kilimo.

Uzinduzi wa ofisi umeongozwa na waziri wa kilimo, Mohammed Bashe, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, na Mkurugenzi Mtendaji, Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo Afrika (AATI), Safia Boly.

Pia katika hafla hiyo ya uzinduzi wa ofisi alikuwepo Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Tanzania, Omar Said, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Shaaban Mudrik Ramadhan Soraga, Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Zanzibar, Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula, Sierra Leone, Henry Musa Kpaka, na washirika waanzilishi wa AATI, Obai Khalifa (Wakfu wa Bill na Melinda Gates), Dkt. Donal Brown (IFAD), Dkt. Agnes Kalibata kutoka Jukwaa la Chakula Afrika AGRA) na Omid Kassiri kutoka kampuni ya McKinsey.