Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equit nchini , Isabella Maganga, amesema kuwa benki yao itaendelea kuwekeza katika mifumo ya kidigitali, kupanua matawi na kuongeza elimu ya fedha kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza sekta jumuishi ya huduma za kifedha nchini.
Akizungumza hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, Maganga, amesema Equity inaendelea kuimarisha ubunifu ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora na nafuu zaidi.
Amesema katika kuadhimisha wiki hii ya huduma kwa wateja benki yao inaendelea kuwekeza katika mifumo ya kidigitali na kuendelea kuwa wabunifu kuhakikisha kwamba jamii inatumia mifumo ya kidigitali katika kupata huduma za kifedha.

“Tumejikita zaidi katika kupanua matawi yetu kuhakikisha kwamba tunafikia wateja wengi zaidi na tunafikia jamii kubwa kwa ujumla. Katika kufanya hivyo inaendana sambamba na kutoa elimu ya fedha na kuhakikisha wale ambao bado hawajafikiwa na huduma za kifedha basi tunawafikia.

“Hivyo kupitia njia za kidigitali na matawi mapya yatakayofunguliwa katika maeneo mbalimbali ya nchi,”amesema Maganga amesema kaulimbiu ya mwaka huu, “Mission is Possible,” inaakisi dhamira ya benki hiyo katika kuwawezesha wateja wake kufikia mafanikio ya kifedha na kibiashara.
Amesema Equity imekuwa mstari wa mbele katika kukuza ujumuishaji wa kifedha kupitia bidhaa rafiki zisizo na makato makubwa, ambazo zinamwezesha Mtanzania wa kipato cha chini kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara wa Equity Bank Tanzania, Prosper Nambaya,amesema benki hiyo inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma kwa kuongeza matawi mapya, kuimarisha huduma za internet banking, na kuongeza mawakala wa kibenki hadi kufikia zaidi ya 3,000 nchi nzima.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya GSM ,Benson Maenya ambaye ni miongoni mwa wateja wa benki hiyo amesema Equity imekuwa mshirika muhimu katika kupanua biashara zake ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, kutokana na mtandao mpana wa kimataifa na huduma bora kwa wateja.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako