March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Nchimbi aendelea kusaka kura za CCM

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Tabora

MGOMBEA mwenza kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amehitimisha mikutano yake ya hadhara ya kampeni katika Mkoa wa Tabora,huku akiwaomba wananchi mkoani humo ifikapo Oktoba 29,wampigie kura mgombea urais wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wake.

Dk.Nchimbi amezungumza hayo Oktoba 6, 2025,mkoani Tabora ambapo katika mikutano ya kampeni mbali ya kuwaombea kura wagombea wa CCM pia amenadi sera na ilani ya uchaguzi mkuu ya chama hicho,ambapo amesema imelenga kuleta maendeleo ya watanzania.

Pamoja na mambo mengine,Dkt.Nchimbi aliwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa Jimbo la Igalula, Ndugu Juma Ramadhan Mustafa [KAWAMBA) pamoja na Madiwani.

Awali kabla ya kuanza kuzungumza na wananchi wa Tabora,Dkt.Nchimbi,alisimikwa kuwa msaidizi wa Mtemi kimila na viongozi wa kimila wa Unyanyembe mkoani Tabora,kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni mkoani humo,Kata ya Kigwa Jimbo la Igalula, wilayani Uyui nakupewa jina la “NYUNGU YA MAWE”.

Hata hivyo Mkoa wa Tabora imekuwa wa 18 ambao Dkt.Nchimbi,amefika tangu CCM,kuzindua kampeni hizo Septemba 28,2025 jijini Dar-es-Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi kwa wagombea wa chama hicho ikiwemo za Urais,Wabunge na Madiwani.