Na Esther Macha,Timesmajira Online,Mbeya
KATIKA kuhakikisha mifugo inachanjwa wafugaji wametakiwa kutoa ushirikiano wa karibu kwa maafisa mifugo wa kata ili kuweza kufanikisha zoezi hilo pasipo vikwazo.
Hayo yamesemwa Agosti,18,2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Dinday Njile aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji chanjo kwa mifugo.
Amesema katika kufanikisha zoezi hilo wafugaji wote wanapaswa kuchanja mifugo yao na kutoa ushirikiano pindi maafisa mifugo wa kata wanapofika katika maeneo yao ili kurahisisha kampeni ya kuchanja mifugo iweze kufanikiwa pasipo changamoto yeyote.
“Kampeni hii ya utoaji chanjo ya homa ya mapafu kwa ng’ombe, imeanza Leo katika Kata ya Mjele kijiji cha Chang’lombe Wilaya ya Mbeya imani yetu wafugaji wote mtazingatia zoezi hili muhimu “amesema .
Pia Njile amewatoa hofu wafugaji kuwa zoezi hilo ni endelevu na litaendelea kwa kipindi cha miaka mitano, hivyo hawapaswi kuwa na wasiwasi.
Hata hivyo amesema Serikali imesikiliza changamoto zinazowakabili wafugaji na tayari imeanza kuzifanyia kazi kwa maslahi ya sekta hiyo muhimu ya mifugo.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi