Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
MGOMBEA Udiwani kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)Kata ya Utengule Usongwe Wilaya ya Mbeya,Aida Haule amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo huku akitaja vipambele vinne akishinda.
Ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja kushirikiana na serikali pamoja na wananchi ili kujenga Vyumba vya madarasa na kuhakikisha Mji wa Mbalizi unakuwa Mamlaka kamili tofauti na sasa ambapo inatamkwa kwa maneno .
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 19,2025 ,baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Udiwani kata ya Utengule Usongwe amesema kata hiyo imekuwa na changamoto ya muda mrefu ya kutokuwa na Mamlaka kamili na kusema mamlaka iliyopo ipo kwa kutamka lakini bado inaitwa kwa jina tu.
“Hii kata ina kilio cha muda mrefu hivyo natarajia viongozi wetu ngazi ya chama na kitaifa iwafikirie wananchi wa kata hii kwani mpaka sasa kuna kilometa mbili tu za barabara ya lami,”amesema.



More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi