March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Walimu wa Madrasa waaswa kuendeleza maadili kwa vijana wao

Na Bakari Lulela,Timesmajira

UMOJA wa walimu wa madrasa (UMAKITA) wamepatiwa semina elekezi  ambayo ni kitovu cha kubadilisha mitazamo mbalimbali ya kampeni rudusha maadili ndani ya dini  na kwenye jamii ya watanzania.

Semina hiyo  imeandaliwa na Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) katika kitengo cha idara ya elimu mahakama ya kadhiJijini Dar es salaam 

Akizungumza hayo jijini Dar es salaam kwenye tukio maalumu Naibu kadhi Sheikh Ally Ngaruko amesema walimu mnawajibu mkubwa wa kuwaelimisha vijana wenu kufuata namna bora ya kutekeleza majukumu yao kwa kuisomesha dini ya mungu na kutanguliza maadili kuwa ni sehemu ya maisha.

“katika kampeni ya rudisha maadili kwa jamii  nyinyi walimu wa madrasa ambao ndio viongozi kwa vijana wetu mnatakiwa kutumia mifano bora  ambayo aliweza kuishi mtume wetu Muhammad dhidi ya kuueliisha umma wa uislamu ,” amesema Ngaruko 

Aidha Naibu kadhi huyo amesema kuwa chimbuko la vijana, watoto hawa ni wazazi hivyo kuna kila sababu ya kuwafunza ama kuwaelekeza namna ya kufuata maadili mema na kutumia vyema Mitandao ndani ya jamii ya watanzania na Taifa letu kwa ujumla .

Kwa upande wake  Maalumu  wa makosa ya kimtandao Yussuph Kileo amesema  kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wetu wanaharibiwa kupitia taknolojia ya Mitandao ya kijamii na kupekea kutumia vibaya na kusababisha taharuki kubwa ndani ya jamii yetu.

Ameeleza kuwa walimu wa madrasa kuwa ndio vioo vya mabadiliko ndani ya jamii kwa nafasi zenu mtumie vema nafasi hiyo katika kuwafunza maadili bora kwa vijana wetu ambao hao baadaeni ndio watakuja kuwa viongozi ama walimu bora katika kuongoza vijana ama watoto wengine siku za usoni.

Hata hivyo kutokana teknolojia simu zinaweza kutumiwa vizuri lakini simu pia zinaweza kutumiwa vibaya hivyo kuna kila haja na sababu walimu wa madrasa kutumia taaluma ya kidini kwa weledi kwa kuwafundisha namna bora ya kuwafunza kilicho bora watoto wetu.

Hivi karibuni tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais , Wabunge na Madiwani hivyo ni vyema kwa vijana kufuata utaratibu mzuri wa kuwachagua viongozi wetu katika namna bora na sifa ya kuiongoza nchi yetu kwa kufuata msingi bora ya amani na usalama kidemokrasia kwa watu wote.
Â