Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Dar-es- Salaam)
SHULE ya Sekondari Zanaki wajivunia mafanikio katika ufaulu ambapo matokeo ya kidato cha sita jumla ya wanafunzi 44 wamepata daraja la kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari,jijini Dar-es-Salaam,Mkuu wa shule ya sekondari Zanaki, Delvine Koka,amesema ni shule hiyo iliyopo wilayani Ilala,imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kutokana na jitihada na ushirikiano wa walimu wa shule hiyo,wanafunzi na wazazi ambapo wamekuwa wakifanya mitihani mbalimbali ya upimaji kila wakati.
“Matokeo ya mwaka huu ya kidato cha ufaulu daraja A wanafunzi 44,daraja la pili 63,daraja la tatu 27 n a daraja la nne mwanafunzi mmoja,”amesema Delvine.
Mwalimu Delvine,amesema katika shule yake wameondoa alama 0 huku lengo ni kuondoa daraja la nne.Huku ikiwa imefanikiwa kuongeza ufaulu katika masomo ya geography,kiswahili,kiingereza,economics na advanced mathematics.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI