Na Irene Clemence ,Timesmajira
NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria,Jumanne Sagini amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria, ya Mama Samia Legal Aid imeleta matokeo chanya na serikali imeridhishwa na utolewaji wa huduma hiyo.
Sagini ameyabainisha hayo alipotembelea Maonesho ya 49 ya kimataifa ya biashara Sabasaba Jijini Dar es salaam (DIFT) yanayoendelea
“Wizara ya Katiba na Sheria inalifanya jambo hili kuwa endelevu kwa kupeleka maafisa ngazi ya Halmashauri ambapo wanawasaidia wananchi kwa kushirikiana na taasisi zingine za kisheria,”amesema Sagini
Amesema uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria wa mama Samia illegal Aid umeonesha huduma hiyo ni hitaji la wananchi.
“Licha ya migogoro ya Ardhi,pia kuna migogoro ya ndoa ambapo Elimu inatakiwa kutolewa kwa kushirikiana na maafisa walipo kwenye Mamlaka ngazi za Mitaa na wataalamu wa msaada wa kisheria waliopo ambao ni wadau wa huduma za msaada wa kisheria kwa kuelimisha wananchi kuhusu ndoa”amesema Sagini

Pia aliwaomba wananchi kutembelea banda la Katiba na Sheria ili kupata elimu inayohusu masala ya Sheria.
Aidha ameishukuru Serikali inayoingozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya maboresho yaliyofanywa katika viwanja hivyo.

.
Katika hatua nyingine Sagini ameipongeza Wizara ya katiba na Sheria kwa kuibuka mshindi wa kwanza kundi la Wizara zote zilizoshiriki maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2025 .
Amesema Wizara hiyo inastahili kuwa washindi wa kwanza ambapo wananchi wameridhishwa na utolewaji wa huduma.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi