Na Judith Ferdinand,Mwanza
IMEELEZWA kuwa kukosekana kwa miundombinu bora huchangia ukosefu wa maendeleo ambapo kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais John Magufuli kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula wamefanikiwa kujenga barabara katika Kata ya Buswelu na bado wanaendelea.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za kuomba kura kwa wananchi wa Kata ya Buswelu uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Buswelu katani hapo mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ilemela DKt.Angeline Mabula,amesema wakati wanaingia madarakani mwaka 2015 kata hiyo ilikuwa haina barabara yenye lami.
Lakini ndani ya miaka mitano wamefanikiwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Nyakato Steel hadi Tx-Igombe yenye urefu wa km18.2 ambayo imeisha jengwa takribani km 5 anaimani inakwenda kukamilika ndani ya kipindi cha Dkt.John Magufuli endapo watachagua wagombea kwa ngazi zote wanaotokana na CCM.
Amesema,barabara yenye urefu wa km 9.2 kutoka Sabasaba kupita kiseke kuja Buswelu ambayo imewekewa na taa za barabarani zinazisaidia watu kufanya biashara mpaka usiku bila shida yoyote inekamilika.
“Kama hiyo haitoshi kuna barabara ya Busanda-Cocacola zaidi ya kilomita 3.38 ambayo nayo inaenda kujengea,tayari fedha zimetengwa za ujenzi wa barabara ya Buswelu-Kiseke Buyombe hivyo tuchagueni sisi wagombea wa CCM ili tutwende tukatekeleze na kukamilisha haya,” amesema Dkt.Angeline.
Pia amesema,kulikuwa na changamoto kubwa ya vivuko Kigala na Lagos zaidi ya milioni 112.2 tayari zimejenga madaraja hayo kwa ajili ya kuvukia na sasa hakuna changamoto hiyo,wanaenda kujengewa kituo cha afya katika kata hiyo huku zahanati ya Nyerere inaendelea kuboreshwa zaidi ili iendane na hadhi ya Baba wa taifa.
Hata hivyo amesema suala la umeme katika jimbo hilo ulikua unapatikana kwa asilimia 35 sasa ni 75 bado 25 ambapo zaidi ya bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya kumalizia maeneo ambayo hayajapata umeme ikiwemo kata ya Buswelu pia katika sekta ya elimu wamejenga madarasa na madawati.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango