Na Queen Lema,Timesmajiraonline,Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewaomba madiwani pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuwa mabalozi wazuri wa kuelezea miradi mikubwa ambayo imetekelezwa na serikali.
Amesema endapo watu kama waliokuwa madiwani wataenda Kuelezea kwa wananchi Kwa ufasaha kabisa miradi iliofanyika itaweza kuruhusu wananchi kuendelea kuiamini serikali yao.
Makonda ameyasema hayo Juni 20,2025 wakati akifunga rasmi baraza la madiwani wa Jiji la Arusha ambapo pia Makonda alitumia mkutano huo kuweza kutoa shukurani kwa madiwani pamoja na aliyekuwa Meya wa Jiji hilo Max Iraqhe.
Alisema ni wakati sahihi sasa wa kuhakikisha kuwa kila aliyekuwa Diwani wa Baraza hilo kusemea vyema miradi ikiwa ni pamoja na kusema thamani halisi ya miradi hiyo.
“Tuwe wazalendo na nchi yetu lakini pia tuhakikishe kuwa yale tulioyaona lakini pia kuyafanya na kupitisha bajeti humu ndani na kisha yakatekelezwa basi tuyaseme tena hadharani kila Mtu aweze kuyajua na kutambua “aliongeza Makonda

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi