Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo,amesema Wilaya yake ya Ilala wanaendelea kung’ara katika sekta ya michezo kwa kuibuka kidedea mwaka 2025 katika mashindano ya Umoja wa shule za Sekondari (UMISSETA) Kanda ya Dar es Salaam.
Mpogolo amesema hayo wilaya ya Ilala,Juni 12,2025 wakati wa kukabidhiwa vikombe 19 vya mashindano ya UMISSETA ambapo Wilaya ya Ilala wamekuwa mabingwa wa mkoa.
“Natumia fursa hii kumpongeza Afisa Elimu Halmashauri ya jiji la Dar es,Mwalimu Mussa Ally na Idara ya Elimu Sekondari kwa kushirikiana na Wakuu wa shule wote na wanafunzi kwa kazi kubwa mliofanya mpaka kuiletea heshima Wilaya ya Ilala sekta ya michezo ni faraja kubwa katika wilaya yetu,”amesema Mpogolo.
Mpogolo amesema jitihada za walimu, wakuu,wanafunzi imefanya wilaya hiyo kungara zaidi ,ambapo aliwataka huko mbele wakafanye vizuri katika mashindano ya ngazi ya Taifa.
Aidha alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa kuleta fedha nyingi katika viwanja vya michezo ikiwemo kuutengeza uwanja wa kisasa shule ya sekondari Benjamini Mkapa .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya akikabidhi vikombe 19 vya UMISSETA,amepongeza idara ya elimu Sekondari,Jiji Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata kwa kuleta heshima Ilala.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mwalimu Mussa Ally,alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa jiji,Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala na Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano wao kuiwezesha Halmashauri hiyo kufanya vizuri katika sekta ya michezo.
Mwalimu Mussa pia alitumia fursa hiyo, kuwapongeza walimu wake kwa mafanikio makubwa katika sekta ya michezo ambapo wilaya ya Ilala imefanikiwa kuunda timu ya mkoa Dar es Salaam aimbayo sasa inajiandaa kwenda kushiriki mashindano ya UMISSETA Taifa.





More Stories
TFF yatinga na safu tatu mpya
Mkazi Kisarawe ashinda Mil. 100, Kampeni ya ‘Tunasherehekea Pamoja’
Ajinyakulia Mil. 5/- Kampeni ya Yas ‘tunasherehekea mwaka mmoja’