Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,ameongoza mamia ya waombolezaji, kutoaji wa heshima za mwisho na mazishi ya Mzee Silvin Mongella, mwenza wa mmoja wa viongozi waandamizi wastaafu nchini, Getrude Mongella.

Shughuli hiyo ya mazishi ya Mzee Mongella, ambaye ni baba mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Mongella,imefanyika Juni 7,2025,Kabusungu wilayani Ilemela mkoani Mwanza,yalitanguliwa na misa takatifu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, ikiongozwa na Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, huku mahubiri yakitolewa na Padri George Nzungu.
Balozi Nchimbi amemuelezea Mzee Mongella kuwa, enzi za uhai wake alikuwa mtu wa kupigania haki za wanawake ndani na nje ya nchi, huku akielezea matunda yake ni kupata viongozi wengi wanawake nchini akiwepo Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Balozi Nchimbi,amesisitiza juu ya mahubiri yaliyotolewa na Padri George Nzungu,juu ya watu kuishi kwa upendo na amani na si kuishi kwa kujivunia mali na nyadhifa walizonazo.
Mbali ya Balozi Dkt. Nchimbi, viongozi wengine waliojumuika pamoja na waombolezaji katika mazishi hayo ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, mawaziri, viongozi waandamizi wa chama na Serikali, wabunge na viongozi wa kiroho kutoka madhehebu ya dini mbalimbali nchini.
More Stories
Kiongozi wa Mwenge awataka RUWASA kukamilisha mradi wa maji kwa wakati Kilindi
Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mama yake mzazi
Sheikh Kabeke asisitiza maadili na amani kuelekea uchaguzi 2025