YAS yatoa Elimu ya mtandao Karibu Kill Fair ,yajipanga kuinua sekta ya utalii
Na Joyce Kasiki, Timesmajira Online – Arusha
MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Wateja Wakubwa na Serikali kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya YAS, Anatori Lelo, amewaasa wananchi wa Jiji la Arusha na wageni wote wanaotembelea Maonesho ya Utalii ya Karibu Kilifair, kuchangamkia huduma mbalimbali za kimtandao zinazotolewa na kampuni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Juni 6, 2025, katika viwanja vya maonesho hayo vilivyoko Kisongo Magereza jijini Arusha, Lelo amesema ushiriki wao katika maonesho hayo ni sehemu ya mkakati wa kuwasogezea wananchi huduma za mawasiliano na kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya mitandao.
“Tumeamua kushiriki katika maonesho ya Karibu Kilifair kwa sababu yanawaleta pamoja wadau wengi wa sekta ya utalii, sekta ambayo sisi kama YAS tunaisapoti moja kwa moja kupitia huduma zetu za mawasiliano na teknolojia ya mtandao,” amesema Lelo.
Ameeleza kuwa kampuni ya YAS inatoa huduma mbalimbali kwa hoteli, makampuni na taasisi nyingine kupitia huduma za ‘connectivity’na mawasiliano ya ndani na nje ya nchi.
“Kupitia ushiriki huu, tunapata fursa ya kukutana ana kwa ana na wateja wetu, kuelewa changamoto zao na kutoa suluhisho papo kwa hapo,” ameongeza.
Mbali na kutoa huduma hizo, Lelo amesema kampuni hiyo inatumia jukwaa hilo kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi salama na yenye tija ya mtandao wa YAS, hususan kwa wafanyabiashara wa sekta ya utalii ambao wanategemea sana mawasiliano katika shughuli zao za kila siku.
Aidha, YAS imejipanga kutatua changamoto za kimtandao zinazowakabili wananchi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya upatikanaji wa huduma kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha na kwingineko, huku wakitoa suluhisho la haraka kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Amesema,maonesho ya Karibu Kilifair yanayofanyika kila mwaka jijini Arusha ni miongoni mwa matukio makubwa ya kimataifa ya utalii, yanayowaleta pamoja wadau kutoka ndani na nje ya nchi huku akisema, Ushiriki wa kampuni kama YAS ni ushahidi wa jinsi sekta ya teknolojia inavyoshirikiana na utalii kukuza uchumi wa Taifa.
More Stories
Shekhe Mavumbi ahamasisha waislamu kupiga kura
Naibu Waziri Nderiananga awasilisha salamu za pole msiba wa mdogo wake Lukuvi
Kiongozi wa Mwenge apongeza wananchi kupelekewa huduma ya maji Handeni