Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KATIKA kuhakikisha wanawake wajasiriamali na Mama Lishe wanapata huduma iliyo bora mkoa Morogoro, Kampuni ya Coca-Cola Kwanza imekabidhiwa eneo maalumu katika Stendi ya Msamvu kwa ajili ujenzi wa soko mkoani humo.
Hafla ya makabidhiano ya eneo hilo maalumu kwa ajili ya soko ilifanyika katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro.
Katika tukio hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,Emmanuel Mkongwa alikabidhi rasmi eneo hilo kwa kampuni hiyo ya Coca-Cola Kwanza kwa ajili ya kuanza ujenzi wa soko maalum.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuimarisha wanawake wajasiriamali na kuchangia maendeleo ya kijamii katika Manispaa ya Morogoro.
Katika hafla hiyo, pia walihudhuria maafisa waandamizi kutoka Manispaa ya Morogoro pamoja na wawakilishi wa Coca-Cola Kwanza.




More Stories
STAMICO yaimarika, yatekeleza kwa vitendo falsafa ya 4R
Ndejembi aridhishwa na ujenzi wa Kituo cha Umeme Iganjo
Wizara ya Viwanda yabainisha utendaji wa taasisi zake