Na Penina Malundo,Timesmajira
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania ,Sheikh Ponda Issa Ponda akabidhiwa rasmi kadi ya heshima ya Maalim Seif ya Chama cha Act Wazalendo huku akisisitiza kuchangia nguvu katika Operesheni ya ACT Wazalendo ya Linda Demokrasia, inayolenga kurejesha haki, uwazi, na usawa katika michakato ya uchaguzi nchini Tanzania.

Sheikh Ponda amekabidhiwa Kadi hiyo leo Jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu mbele ya viongozi wengine waandamizi wa Chama hicho pamoja na Ngome zake.
Mbali na Kadi hiyo pia amekabidhiwa Katiba ya Chama hicho kama kitendea kazi chake katika harakati zake za siasa ndani ya Chama .



More Stories
Safiri nchi 190 ukiwa umeunganishwa na Kwetu eSIM
Devotha ataka mali kusajiliwa dhamana ya mikopo
Yas yawashika mkono mama wajawazito Hospitali ya Ubungo