Na Patrick Mabula, Kahama.
SERIKALI wilayani Kahama imesema inafanya uchunguzi juu ya tukio la miili ya watu wanne waliouawa kisha kutupwa katika mto uliopo kijiji cha Mwabomba kata ya Idahina halmashauri ya Ushetu na kukutwa ikiwa imeharibika vibaya ili sheria ichukue mkondo wake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama , Anamringi Macha alisema miili ya watu hao waliouawa na watu wasiojulikana ilibainika jumapili iliyopita katika mto huo uliopo karibu na machimbo ya dhahabu ya Mwabomba ikiwa imeharibika vibaya huku sura zao kutotambulika .
Macha alisema serikali kwa kutumia vyombo vyake vya dola inafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu waliofanya kitendo cha mauaji hayo na kuitupa miili hiyo katika mto huo unaotenganisha wilaya ya Kahama na wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti