▪️Waziri Mavunde awapongeza RC Mtanda,Kamati ya Usalama,Uwanja wa Ndege na Kikosi kazi Madini
▪️Aelekeza uchunguzi zaidi kubaini mtandao wote wa wahusika
▪️Atoa rai kwa wadau wa madini kuzingatia sheria ya biashara ya madini nchini
▪️Raia wa Kigeni mwenye asili ya India ashikiliwa
Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari ljumaa usiku,Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda,Vyombo vya usalama,uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya.
“Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu
Katika tukio hilo,almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67) yaligunduliwa yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.
Nitoe rai kwa wadau wote wa Sekta ya Madini nchini kuhakikisha wanafuata sheria ya biashara ya madini nchini Tanzania ili wasipate hasara kwa kupoteza madini hayo ambayo hutaifishwa na serikali” Amesema Mavunde
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.
More Stories
TAZAMA PIPELINE yalishika mkono jeshi la polisi Mbeya
Vyama vya Ushirika Katavi vyatakiwa kuthibiti utoroshaji mazao
Suluhu mgawanyo wa mapato wa huduma za usafiri wa anga nchini, wapatikana