December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Team Moses yaanza vizuri mashindano ya Hoopers

TIMU ya mpira wa kikapu ya Moses ‘Team Moses’ imefanikiwa kuanza na ushindi wa vikapu 64 kwa 51 dhidi ya ‘Team Seta’ katika mashindano ya kuwania kitita ch Sh. milioni 1 katika mashindano yaliyoandaliwa na Hoopers yanayofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Arusha, Njiro.

Timu hiyo ya Hooperz imeandaa mashindano hayo kwa ajili ya kuendeleza na kuvikuza vipaji vya vijana wao ambao wamekua wakiwafundisha kwa miaka mingi sana.

Mbali na vijana, Hoopers wamechanganya na wakongwe ili kuwarithisha baadhi ya uwezo walionao huku lengo lingine likiwa ni kuwapa nafasi wanawake kwa maana kila timu ni lazma iwe na wanawake ambao ni lazima wacheze.

Mashindano hayo yanashirikisha timu nne zilizokuwa zikifanya mazoezi katika uwanja mmoja ambazo zote zilikuwa zikiundwa kwa taribani miaka minne ili kuja kushiriki

Mratibu wa Chama cha Kikapu Kanda ya Kaskazini, Bariki Kilimba ameuambia Mtandao huu kuwa, katika mashindano hayo kuna wachezaji 12 ambao wanatoka katika timu ya wanawake ambao wamegawanjwa katika timu hizo nne.

Timu hizo nne zinacheza kwa mfumo wa mzunguko ambapo kila timu itacheza mechi tatu na baada ya hapo mshindi wa kwanza atacheza na mshindi wa tatu na mshindi wa pili atacheza na mshindi wa nne.

Kilimba amesema kuwa, baada ya kumaliza hatua hiyo, timu zitakazoshika nafasi ya kwanza nba ya pili zitakutana katika mchezo wa fainali ambapo zitachezwa mechi tatu ‘Best 3 game’ huku watakaoshika nafasi ya tatu na mme wakichuana kumpata mshindi wa tatu.

“Baada ya kuunda timu hizi kwa takriban miaka minne tuliona bora kuandaa mashindano ili kutoa chamngamoto kwa wachezaji wetu lakini pia kupata timu bora itakayoweza kuiwakilisha Hoopers kwenye Ligi ya Mkoa msimu ujao. Lakini pia ili kukuza kikapu kwa wanawake tumeamua kugawa wachezaji watatu kwa kila timu, ” amesema Kilimba.

Katika mashindano hayo, yanayofanyika kila mwisho wa wiki, mshindi wa kwanza atapata kitita cha Sh. milioni 1, mshindi wa pili ataondoka na Sh. 500,000, MVP atapata Sh. 100,000, Mlinzi bora ataondoka na Sh. 50,000 pamoja na zawadi nyingine za makombe.