Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
BENKI ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu imetoa msaada wa bati 120 zenye thamani ya Mil. 5 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la watoto wa kike shule ya Sekondari Usongwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika kuunga mkono serikali ya awamu ya sita upatikanaji wa huduma bora za elimu hapa nchini.
Mbali ya kukabidhi bati hizo pia Benki hiyo imekabidhi kompyuta tano za kujifunzia kwa shule ya Sekondari Iziwa iliyopo halmashauri ya Jiji la Mbeya,
Akizungumza Machi 20,2025 wakati wa kukabidhi msaada huo wa bati kwa shule ya Sekondari Usongwe pamoja na Kompyuta tano za shule ya Sekondari Iziwa
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za juu,Wogofya Mfalamagoha amesema kuwa changamoto za sekta ya elimu Tanzania kwa Benki ya NMB ni jambo la kipaumbele na kuwa kutokana na ukweli kwamba elimu ndio kipaumbele kikuu kwa maendeleo
Mfalamagoha amesema kuwa benki hiyo inatambua serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia elimu Bora kwa nguvu zote katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu mjini na Vijijini
Tulipopata maombi ya kuchangia maendeleo ya elimu katika Shule hizi tuliamua mara moja kuja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya sekta hii muhimu kwa jamii yetu kama Benki ya NMB tunao wajibu wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayopata amesema Meneja huyo wa Kanda
Aidha Mfalamagoha amesema benki hiyo kwa miaka mingi pia imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye elimu ikiwemo madawati vifaa vya kuezeka,vitanda,magodoro na vifaa vingine vya kusaidia matibabu, na majanga yanayoipata nchi
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Mohamed Fakil ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Mbeya amesema kuwa benki ya NMB ni wadau wakubwa na kusema serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu kusema wadau wapo kwa ajili ya kusaidia na kuchochea maendeleo kwenye maeneo ambayo serikali kwa upande wake imeshindwa kukamilisha ndo sababu matatizo yapo na yakiisha hakutakuwa na sababu ya kuongeza kuendelea kutoa msaada.
“Mwaka jana tulitangaza madarasa kukamilika lakini baada ya kutangaza kukamilika lakini wanafunzi wa kidato cha kwanza wameongezeka mara mbili yake maana yake ni lazima madarasa yaongozek ndo maana watumishi wameendelea kuajiliwa ili watatue matatizo yaliyopo kwa hiyo sisi tunategemea leo mmeleta bati kesho mtakuja kukarabati ukumbi wetu huu tuliokaa haufanani na hadhi ya shule ambayo haitoi ufaulu mbaya
Mkuu wa shule ya Sekondari Usongwe,Mwl. Varelia Mtega amesema kuwa wamepokea bati bando 11 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wa kike ambayo ilikuwa ahadi ya Benki ya NMB katika mahafali ya kidato cha sita may Mwaka jana.
Ofisa Elimu wilaya ya Mbeya Aliko Mbuba amesema kuwa Misaada inayotolewa na Benki ya NMB kitaaluma wanaendaelea kuboresha elimu Usongwe na kwamba kwa mkoa wa Mbeya Usongwe Sekondari ndo shule inayofanya vizuri .


More Stories
Wananchi waaswa kutoa taarifa vitendo vya ukiukwaji haki za binadamu
Mvua ilioambatana na upepo yasababisha maafa Kata ya Namanyere
Tanesco,Kanona wakutana kwa mazungumzo ya awali ya biashara ya mauziano ya umeme