Na Penina Malundo,TimesMajira ,Online
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) , leo imefungua rasmi dirisha la udahili wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/21.
Udahili huo unatarajia kuanza leo rasmi hadi Septemba 25 mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa TCU,Prof.Charles Kihampa amesema dirisha hilo limefunguliwa leo badala ya Agosti 31,2020, tarehe iliyokuwa imepangwa hapo awali kutokana na matokeo ya kidato ya sita kutoka .
Amesema utaratibu wa maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo kwa mwaka 2020/21,utahusu makundi makubwa matatu ya waombaji ikiwemo wenye sifa stahiki za kidato sita,wenye sifa stahiki za Stashahada (Ordinary Diploma) na wenye sifa stahiki za Foundation Programme ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
“Ili kufahamu sifa stahiki kwa makundi matatu yaliyotajwa hapo juu,waombaji wanaelekezwa kusoma vigezo vilivyooneshwa katika kitabu cha mwongozo cha TCU,”amesema
Wakati huo huo Prof.Kihampa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini.
Amesema maonesho hayo yanatarajia kufanyika kuanzaia Agosti 31 hadi Septemba 5 mwaka huu ambapo yatapata fursa ya wananchi kuonana ana kwa ana na Vyuo vya elimu ya juu.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo