Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Morogoro
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, wamekutana mkoani Morogoro,kujadili na kupitisha bajeti ya bodi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2025/26.
Akiongea na Waandishi wa Habari mkoani humo,Machi 4,2025,Mwenyekiti wa Baraza hilo na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara,Mhandisi Rashid Kalimbaga, amesema bajeti hiyo imezingatia majukumu ya bodi kwa kutoa kipaumbele kwenye uanishaji wa vyanzo vipya vya mapato ya mfuko.

Pia ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za matengenezo ya barabara zinazopelekwa kwa Wakala za Barabara nchini (TANROADS na TARURA) pamoja na kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwa ajili ya matengenezo ya barabara zinapelekwa kwa wakati kwa wakala wa barabara,ili mtandao wa barabara nchini wenye jumla ya kilomita 188,000 uweze kupitika majira yote ya mwaka.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Mapato wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Godlove Stephen, amesema kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 imejikita katika kufanya tafiti mbalimbali zitakazowezesha upatikanaji wa vyanzo vipya vya mapato ya Mfuko wa Barabara.
Hali itakayosaidia kuongeza uwezo wa mfuko huo kugharamia mategenezo ya barabara nchini, kuimarisha usimamizi wa makusanyo yatokanayo na hifadhi za barabara pamoja na kuboresha matumizi yake kwa lengo la kuongeza fursa za ajira na kipato kwa Watanzania watakaopenda kutumia hifadhi za barabara kufanya biashara mbalimbali kwa ajilia ya kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Rehema Lungo, akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara,amesema kama watumishi wanajipanga kwa ajili ya kuandaa mpango kazi sambamba na kuainisha manunuzi yote kwenye mfumo wa manunuzi wa NeST kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa bajeti hiyo ifikapo Julai 1, 2025.
More Stories
Muhimbili:Tanzania ya kwanza kutumia mtambo unaotumia tiba hewa Afrika Mashariki na Kati
PURA yaendelea kunadi vitalu 26 vya gesi asilia,mafuta
Wanawake wametakiwa kuhakikisha wanampa kura za heshima