


Na Agnes Alcardo, Timesmajiraonline. Dar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili mkoani Tabora leo Desemba 19, 2024 na kupokelewa na viongozi mbalimbali ikiwemo wa kichama wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Nkumba.
Balozi Nchimbi amewasili mkoani humo kwa ajili ya ziara yake ya kichama itakayofanyika kwa siku mbili, ambapo pia amepata nafasi ya kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa Chama kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Wilson Nkhambaku.
Pia, amepata taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha.
More Stories
The Desk and Chair yatoa vifaa saidizi kwa Masatu na mkewe
jengo la mama,mtoto la bilioni 6.5 lazinduliwa Mbulu
Dkt.Malasusa ataka hospitali ya Haydom kuombea wafadhili wanaoishika mkono