


Na Agnes Alcardo, Timesmajiraonline. Dar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili mkoani Tabora leo Desemba 19, 2024 na kupokelewa na viongozi mbalimbali ikiwemo wa kichama wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Nkumba.
Balozi Nchimbi amewasili mkoani humo kwa ajili ya ziara yake ya kichama itakayofanyika kwa siku mbili, ambapo pia amepata nafasi ya kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa Chama kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Wilson Nkhambaku.
Pia, amepata taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha.

More Stories
Madale Saccos yakaribia kukamilisha usajili, wanachama wafikia 138
Dkt. Kijaji akutana na WTTC kuhusu uhifadhi na uwekezaji nchini
Dkt.Kijaji akutana na wawekezaji,wadau wa Utalii Uingereza