Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeelezea kusikitishwa na baadhi ya watu wasiofahamika ambao waliwasha moto na kuunguza nguzo nne za umeme katika eneo la Gera Kashasha wilayani Muleba,Kagera.
“TANESCO tunatoa taarifa kuwa, watu ambao bado hawajafahamika wamewasha moto uliosababisha kuungua kwa nguzo nne za kusafirisha umeme eneo la Gera Kashasha wilayani Muleba.Tukio hilo limesababisha baadhi ya maeneo Wilayani Muleba kukosa huduma ya umeme,”imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO makao makuu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wataalamu wa TANESCO na mafundi wakiendelea na kazi ya kurejesha huduma ya umeme, TANESCO kwa kushirikiana na vyombo vya usalama inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwafikisha kwenye vyombO vya sheria wale wote waliohusika.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea