

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Ndugu Patroba Chaulo, (katikati) leo Julai 6, 2024 wakati alipotembelea banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 48 ya Biashara yanaoyoendelea jijini Dar es Salaam. Walio katika sare ni wanafunzi wa CBE walioshiriki Maonesho hayo.






Wadau mbalimbali waliotembelea banda la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),leo Julai 6, 2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara (sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam wakipatiwa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Chuo hicho.
CBE inapatikana katika banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo pamoja na kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi pia wanatoa huduma ya kusajili hapo hapo wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho.
More Stories
Visima 67,000 vya umwagiliaji kuchimbwa nchiniÂ
DC Songea ahimiza matumizi na uwekezaji kwenye nishati safi
PPPC yawanoa wabunge umuhimu wa utaratibu wa PPP kwenye miradi