October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TYC ilivyojipanga kuwainua vijana kupitia miradi yake

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

SHIRIKA linalojishughulisha na masuala ya Vijana  Tanzania  Youth  Coalition (TYS),imejipanga kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata elimu kupitia mitandao mbalimbali ili waweze kukuza biashara zao.

Akizungumza kwenye maonesho ya 48 ya Biasharaya Kimataifa yanayoendelea ,Ofisa Utekelezaji  wa Mradi wa  Boresha  Maisha Vijana  uliofadhiliwa na Shirika la We Effect na kutekelezwa na TYC,Josephine Onesmo  amesema changamoto kubwa ya vijana wanayokutana nayo,ukiachilia mbali suala la mitaji wanakosa kujua ni namna gani wanaweza wakatafuta masoko mbali na eneo ambalo wanaishi.

Amesema mwaka huu wameamua kuwaleta vijana kutoka maeneo mbalimbali katika maonesho ya Sabasaba kwa lengo kuwaunganisha vijana  na fursa mbalimbali ambazo wanazifanya kuweza kupata elimu na kutambua fursa zingine katika  kukua katika masuala ya utunzaji wa fedha,elimu  kuwekeza ,kujiunga na vikundi.

Pia amesema watapata uelewa wa  kujua mifumo mbalimbali ya biashara itakayofanya wakuwe katika masuala ya masoko ya kimtandao katika kukuza biashara zao.

“TYC inawanachama mbalimbali ambao ni taasisi za vijana lakini zinafanya kazi na vikundi vya vijana ambao ni wajasiriamali na vijana wakulima, katika utekelezaji wa mradi huu moja ya malengo ni kuwajengea uwezo vikundi vya vijana wajasiliamari lakini wanachama wa tyc kuwa na mifumo bora ya uendeshaji wa taasisi na vikundi vyao na kupata fursa mbalimbali za kibiashara katika vikundi vinavyofanya ujasiriamali na shughuli za kilimo,”amesema na Kuongeza 

“Sabasaba hii tumekuja na vikundi kutoka Mkoa wa  Iringa na Dodoma ambao ni wanachama wa TYC ,Pia tumekuja na Vijana wajasiliamari kutoka Kilimanjaro ambao wamekuja na bidhaa mbalimbali,”amesema. 

Kwa upande wake Ofisa  Utekelezaji  Mradi wa USAID Kijana Nahodha (YOUNG CAPTAIN) , uliofadhiliwa na USAID na kutekelezwa na  Taasisi ya TMARC-Tanzania  na washirika wenza TYC pamoja na Shirika la Kimataifa  la Care na Ylabs,Salma Kagya amesema vijana nguzo imara katika kujenga taifa hivyo ni vema kuhakikisha wanawekewa mazingira bora.

Amesema vijana ni asilimia kubwa sana Tanzania ambao  wanakiu ya kupata fursa mbalimbali “Mradi huu unawafanya vijana kujitambua zaidi waweze kuwa na afya bora na kuwa na ushiriki bora katika jamii,”amesema.

Amesema  mradi huo wa Nahodha  ni  wa vijana umri kati ya miaka 15 hadi 25  unaoendeshwa katika maeneo matatu Dares Salaam,Morogoro na Zanzibar .

“Mradi huu unajumla ya vijana wanaotarajiwa kufikiwa ni 45000 ambapo ndani ya hiyo vijana hao  wapo katika vikundi wanajiendeleza kiuchumi lakini pia sabasaba  tupo na vijana hao ambao wamekuja na bidhaa ambao wamezibuni  wenyewe,”amesema.

Amesema vijana hao katika mradi huo wamekuja kujitafutia kipato kwa kuuza bidhaa zao  zkama Mkaa Mbadala ,Majiko Sanifu ,bidhaa  ambazo za kidigital i,mafuta ,sabuni za mwani na mafuta ya nazi,picha wachoraji.