October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yatoa Bilioni 2.6 kuboresha huduma za Afya Manyara

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.6 kuboresha huduma za afya ambapo katika kuboresha huduma hizo kuna ujenzi wa majengo ya mama na mtoto, jengo la upasuaji na jengo la maabara katika hospitali ya wilaya ya kiteto iliyopo mkoani Manyara.

Dkt Mollel ameeleza hayo leo wakati alipofanya ziara wilayani humo ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya .

Dkt.Mollel amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ambapo mpaka sasa Wilaya ya kiteto imepokea Vifaa vya shilingi Milioni 185 kutoka Bohari ya Dawa ( MSD) na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo.