October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kocha Namungo aipigia saluti Simba

Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online

KOCHA wa klabu ya Namungo FC Hitimana Thiery amesema, timu yake ina kazi kubwa ya kupambana na Simba kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Namungo FC ilitinga hatua ya fainali baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Sahare All Stars uliochezwa Julai 11, Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Simba wakitinga hatua baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Yanga bao 4-, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kuelekea kwenye mchezo huo, Hitimana amesema anatambua kuwa kuna kazi kubwa kupambana na mabingwa kwenye mchezo wao wa fainali.

“Sio kazi nyepesi kushinda mbele ya mabingwa ambao wapo vizuri na tunawaheshimu kwa kuwa tunawatambua vizuri wapinzani wetu na wanajua kile wanachokifanya.

“Nilikuwepo uwanjani kuona namna ambavyo walikuwa wakipambana ndani ya uwanja, ila hilo halinipi presha nitakiandaa kikosi changu vizuri ili kipate ushindi, ” amesema.